Wakazi wa Mkoa wa Njombe wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zinapelekwa na serikali katika maeneo yao ikiwemo miradi mikubwa ya ujenzi inayoendelea ili kuondoa dhana ya uhaba wa ajira.
Hayo yamesemwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo alipotembelea miradi miwili ya ujenzi wa vyuo vikuu Mkoani Njombe ,Chuo kikuu Huria cha Tanzania (OUT) naChuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kampasi ya Njombe.
Katika ziara hiyo Pro.Nombo amewataka wakandalasi kuongeza kasi ya ujenzi na kuzingatia kanuni ubora za ujenzi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi judica Omari amewahamisha wananchi kuchangamkia fursa za ajira zitokanazo na miradi hiyo ili waweze kujipatia kipato na kushiriki moja kwa moja katika maendeleo ya mkoa.
Ujio wa kampasi hii katika Mkoa wa Njombe unaenda kuondoa adha kwa vijana kusafiri umbali mrefu kufuata elimu ya chuo kikuu, kupoteza muda na gharama za usafiri, ambazo kwa sasa watazitumia kama mitaji
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.