Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF), Afande Mbaraka Semwanza, leo tarehe 2 Desemba 2024, amefanya ziara ya kikazi mkoani Njombe. Akiwasili mkoani hapa, Kamishna Semwanza alipokelewa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi Joel B. Mwakanyasa, na kuelekea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.
Afande Semwanza alipata fursa ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kukaribishwa rasmi na Mhe. Mtaka. Katika mazungumzo yao, Kamishna alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano thabiti ambao ofisi yake imekuwa ikitoa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, akisisitiza kuwa msaada huo umechangia kuimarisha usalama wa wananchi na maendeleo ya mkoa.
Mhe. Mtaka, kwa upande wake, alilipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa juhudi na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake. Alisisitiza dhamira ya kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha usalama wa wananchi na kukuza maendeleo katika mkoa wa Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.