• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

DKT. JUMA MFANGA AONGOZA KIKAO NJOMBE.

Posted on: January 22nd, 2025

Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Juma Mfanga, pamoja na wawakilishi wa UNICEF wakiongozwa na Bi. Ruth Nkurlu, Mtaalamu wa Lishe wa UNICEF, tarehe 22 Januari, 2025 wamekutana kujadili maandalizi ya uzinduzi wa Mpango Harakishi wa Kupunguza Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (Stunting Reduction Acceleration Response Plan).


Mpango huu unalenga kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto, ambao kwa mujibu wa Takwimu za  utafiti wa Afya, Demografia na viashiria vya Malaria Tanzania (TDHS) za mwaka 2022, unaonesha kuwa asilimia 50.4 ya watoto chini ya miaka mitano wamedumaa.


Katika kikao hicho, viongozi walisisitiza umuhimu wa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu lishe bora na kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa familia.


Dkt. Mfanga alieleza kuwa mpango huu utajumuisha afua mbalimbali za kuimarisha afya na lishe ya watoto.


Bi. Nkurlu aliongeza kuwa UNICEF itaendelea kutoa msaada wa kiufundi katika utekelezaji wa mpango huu, ili kuhakikisha watoto wanapata lishe bora na huduma muhimu za afya kwa maendeleo yao.

Uzinduzi rasmi wa " Njombe Region Stunting Reduction Acceleration Response Plan" unatarajiwa kuhusisha viongozi wa Serikali, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.