SEKRETARIETI ya Mkoa wa Njombe imeadhimisha siku ya Afya na Lishe ya Kijiji katika Kata ya Mahongole, Halmashauri ya Mji Makambako na kutoa rai kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya lishe bora kwa ajili ya kukabiliana na Utapiamlo na Udumavu.
Afisa Lishe mkoa wa Njombe, Bi. Betha Nyigu akiongea na wakazi wa kijiji cha Mahongole mkoani hapa alitoa wito kwa wanawake na wanaume kuzingatia afya ya mtoto ili kukabiliana na tatizo linalotokana na udumavu kwa watoto.
Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa, Bi. Betha alisema kuwa katika mkoa wa Njombe hali ya udumavu imefikia asilimia 53.6 na kuufanya mkoa kuwa wa kwanza kitaifa.
“Lengo la kuja katika kijiji cha Mahongole kufanya maadhimisho haya ya siku ya Afya na Lishe ni kuangalia utekelezaji wa mkabata wa lishe katika ngazi ya jamii ambapo moja ya kiashiria kilichopo ni utekelezaji wa siku ya Afya na Lishe,” amesema Bi. Betha.
Aidha Afisa Lishe huyo wa mkoa wa Njombe amesema waliamua kuwafikia wananchi wa kijiji cha Mahongole kwa lengo la kuzungumza na wakina mama na kina baba juu ya changamoto ya utapiamlo pamoja na udumavu ambao unakabili kijiji hicho kwa baadhi ya watoto.
Maadhimisho hayo yalifanyika Oktoba 30, 2019 katika kijiji cha Mahongole, Kata ya Mahongole, Halmashauri ya Mji Makambako, mkoani Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.