Mhe. Anthony Mtaka ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, leo tarehe 24 Aprili2024 amefanya ziara na kukagua Miradi ya Maendeleo ili kujiridhisha na hali halisi iliyopo.
Ziara hiyo ya kikazi imefanyika katika Halmashauri ya Mji Njombe ambapo hapo ametembelea na kukagua ujenzi wa Majengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Yakobi na amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe ambapo hapo amekagua Ujenzi wa Madarasa,Ujenzi wa Bweni la kike na Bweni la Wanafunzi wa kiume.
Aidha, Mhe. Mtaka amewatakia wanafunzi wote wa kidato cha sita maandalizi mema ya mtihani wao ambao utatarajiwa kuanza Kufanywa siku zijazo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.