Hali ya huduma ya Maji Vijijini
Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2019, jumla ya miradi 39 kati ya 54 imetekelezwa. Hali ya utekelezaji ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali lifuatalo
Jedwali Na. 28: Utekelezaji wa Miradi kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2018/19
Halmashauri
|
Miradi iliyopangwa kutekelezwa |
Miradi iliyokamilika |
Miradi inayoendelea kutekelezwa |
Miradi iliopo hatua ya usanifu na manunuzi |
Ludewa DC
|
9 |
5 |
2 |
2 |
Makambako TC
|
9 |
3 |
1 |
5 |
Makete DC
|
12 |
4 |
8 |
0 |
Njombe DC
|
7 |
2 |
1 |
4 |
Njombe TC
|
6 |
1 |
4 |
1 |
Wanging’ombe DC
|
11 |
5 |
3 |
3 |
Jumla
|
54 |
20 |
19 |
15 |
Kukamilika kwa miradi hiyo 20, pamoja na miradi ya Wadau wengine kumewezesha kuongezeka na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo hadi Machi, 2019 wananchi wapatao 375,600 kati ya 564,209 sawa na asilimia 66.57% ya wakazi waishio Vijijini wanapata huduma ya Maji safi na salama.
Hali ya upatikanaji wa Maji katika kila Halmashauri kwa maeneo ya Vijijini ni Njombe (Wilaya) asilimia 60, Njombe (Mji) asilimia 51, Ludewa asilimia 66.7, Makete asilimia 80.9, Makambako (Mji) asilimia 60.8 na Wanging’ombe asilimia 70.14.
Kwa sasa Mkoa unatekeleza awamu ya pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP II) ambapo jumla ya miradi 40 kuanzia mwaka 2018/19 ikiwemo miradi 8 katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Miradi 5 katika Halmashuri ya Mji Makambako, Miradi 9 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Miradi 7 katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Miradi 6 katika Halmashauri ya Mji Njombe na Miradi 5 katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.
Kukamilika kwa awamu ya pili ya Programu ya maendeleo ya Sekta ya maji kutaziwezesha Halmashauri za Mkoa kuongeza wastani wa upatikanaji wa huduma ya Maji kufikia asilimia 85.7 ifikapo mwaka 2020/21.
Katika kuboresha huduma ya Maji ili kuwa endelevu, vyombo huru vya watumiaji Maji (Community Owned Water Supply Organization- COWSOs) 114 vimeundwa na kusajiliwa na vinatoa huduma katika vijiji 145.
Hali ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji
Hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji katika Miji ya Njombe na Makambako na Miji mikuu ya Wilaya za Ludewa, Makete ni wastani wa asilimia 55.75 ambayo ni sawa na watu 97,312 kati ya watu 174,549 waishio katika miji hiyo ambapo Njombe Mjini ni asilimia 61, Ludewa asilimia 49, Makete asilimia 53.37, na Makambako asilimia 61.2 na mradi wa Kitaifa Wanging’ombe 77.4% (Watu wanaopata huduma ni 73,609 kati ya watu 95,068).
Hadi Machi, 2019, jumla ya miradi 5 inaendelea kutekelezwa ili kuboresha huduma ya maji ikiwa ni pamoja na Njombe Mjini ambapo utekelezaji umefikia 95%, Makambako ambapo utekelezaji umefikia 60%, Ludewa ambapo utekelezaji umefikia 98%, Makete ambapo utekelezaji umefikia 75% na Mradi wa Kitaifa Wanging’ombe ambapo utekelezaji umefikia asilimia 85
Kukamilika kwa miradi hiyo kutaziwezesha Mamlaka za Maji na usafi wa Mazingira Mijini kuongeza asilimia ya upatikanaji wa huduma ya Maji kufikia wastani wa asilimia 69.3 (69.3%) na mradi wa kitaifa wa Wanging’ombe asilimia 79.
1. Mkoa umeandaa Mpango wa kukidhi mahitaji ya Maji kwa wakazi wote wa miji hiyo kwa kutekeleza miradi ifuatayo;-
2. Mradi wa Kitaifa wa Wanging’ombe kutokana na chanzo cha mto Mbukwa.
3. Mradi wa Mji wa Njombe kutokana na chanjo cha Mto Hagafilo.
4. Mradi wa Mji wa Makambako kutokana na chanjo bwawa la Tagamenda na visima virefu eneo la Idofi.
5. Mradi wa Mji wa Ludewa kutokana na chanjo cha Mto Ilunga.
6. Mradi wa Mji wa Makete kutokana na chanjo cha Mto Kilambo (usanifu unaendelea).
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.