Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthon Mtaka amefanya ziara ya kikazi leo katika halmashauri ya Mji Njombe Kata ya Ramadhani mtaa wa Mgodechi,Kufuatia kukamatwa kwa shehena ya mifuko ya mbolea inayodaiwa kutumika kufanya uchakachuaji na udanganyifu leo hii, kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Antony Mtaka wamefika kwa wakulima walionunua mbolea siku chache zilizopita na waliokiri kununua mbolea iliyofanyiwa udanganyifu kutoka kwa mfanyabiashara jina lake limehifadhiwa anayeshukiwa kukutwa na shehena hiyo ya mifuko inayokadiliwa kuwa zaidi ya 10,000.
Zoezi hilo limefanyika leo Januari 19, 2023 katika mtaa wa Mgodechi pembezoni kidogo ya mji wa Njombe kukutana na wakulima ambako pia kunapatikana moja ya duka la mfanyabiashara anayedawa kuuza mbolea feki,walisema kuwa mbolea hiyo ilikua na utofauti na mbolea nyingine ambazo wamewahi kutumia.
Ibrahimu kilunde mkulima wa viazi alisema mbolea hiyo ilikua tofauti na mbolea ambazo wamezoea kutumia kwenye msimu uliopita wa kilimo.
"Tulinunua ya kupandia na kukuzia madhara yake nimeyaona,mazao yananyauka kingine hata ardhi yenyewe itapata madhara kwa sababu tumetumia mara kwa mara,kuna mabadiliko ya rangi ina rangi zaidi ya tatu na ya zamani ilikua a rangi moja kama nyeupe ni nyeupe kama nyeusi inakua nyeusi"alisema
Zawadi Mgaya alisema kuwa mbolea hiyo inaujazo mdogo kuliko mbolea nyingine."Mimi nilinunu mifuko minne hadi sasa hivi ninayo nyumbani,ujazo ni mdogo sana ukilinganisha na mifuko mingine ambayo tuliwahi kununua sehemu nyingine"alisema Mgaya.
Kwa upande Adelina Stewele alisema alivyofika dukani aliomba kuuziwa mbolea aina ya DAP mifuko miwili lakini alivyofika nyumbani alikuta iko tofauti.
"Nilivyofika nyumbani wakati nafungua nakuta sio DAP na mbolea yenyewe nimetembea nayo hii hapa"alisema.
Aliongeza kuwa"Hata ujazo haijajaa,mfuko kawaida unashinwa mshono mmoja sasa huu ulikua umeshonwa mara mbili ukiwa umepinda pinda"alisema.
Geresius Ng'ande alisema alinunua DAP mifuko miwili"Wakati naweka kwenye shamba nakuta yani hayeyuki nikauuliza hii safari hii ni mbolea aina gani mbona ni vumbi nikafungua mwengine nao nikakuta ni vumbi kwa hiyo nikashindwa nikakuta habari kwamba vijana wamebaini mbolea feki"alisema Ng'ande.
Exaud Mgina alisema alipokwenda kununua mbolea hiyo aligundua utofauti na alipokwenda kuuliza dukani aliambiwa asubiri atabadilishiwa.
Kufuatia mkutano huo wakulima waliokumbwa na kadhia ya kuuziwa mbolea bandia wakatakiwa kurudi majumbani kwao na kujitokeza na mifuko waliyonunua kwa mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo kulifanyika upimaji wa mbolea hizo na afisa udhibiti ubora wa mbolea TFRA nyanda za juu kusini Chimile Mfugale alibaini majina ya mbolea kwenye vifungashio ni tofauti na mbolea iliyopo ndani ya mfuko huku mbolea nyingine ikiwa na mchanganyiko usioeleweka.
Aidha mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka aliwataka wananchi wote ambao wameuziwa mbolea hizo kujiandikisha majina kwa ajili ya kufanyiwa fidia.
"Jana kwenye nyumba ya huyu mfanyabiashara tulikamata mifuko elfu 10,532 ambayo ilikua ni mifuko imetoka kiwandani ni mitupu lakini yameandikwa majina ya hizi mbolea maana take alikua anafanya kazi ya kupriiti hii mifuko anakuja anachakachua anaandika minjingu kumbe DAP anaandika DAP kumbe minjingu anakuja anauza kernye maduka yake kama zoezi lile lingefanikiwa maana angefanya uchakachuaji wa mbolea kama alivyokua anauza hapa dukani kwa mifuko ile angefanikiwa angepata shilingi milioni 737,240,000"alisema.
Hata hivyo mkuu wa mkoa alisisitiza kutafutwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola mfanyabiashara huyo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.