Mikataba yenye thamani zaidi ya Bil. 22 ya ujenzi wa barabara Mkoa wa Njombe imesainiwa leo,ikiwa ni sehemu ya pili tangu mikataba hiyo kusainiwa Mkoani Dodoma Agosti 14, mwaka huu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) Mkoa wa Njombe,Mhandisi Gerald Matindi katika kikao cha utiaji saini mikataba ya matengenezo na ukarabati wa barabara na madaraja awamu ya pili kwa asilimia 40,kwa mwaka wa fedha 2022/2023,kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Mhandisi Matindi amesema kuwa,lengo la kusaini mikataba hiyo kwa awamu ya pili ngazi ya Mkoa baada ya ngazi ya Taifa ni kuwapa umiliki wa miradi hiyo wananchi wa Mkoa wa Njombe ili waweze kupokea miradi ambayo toka miaka mitatu iliyopita imeongezeka kwa asilimia 37.
Amesema kuwa,kupitia mikataba hiyo TARURA kwa mwaka huu wa fedha itafanikiwa kukamilisha matengenezo ya barabara zenye jumla ya kilomita 1175.7,ambazo ni kilomita 8.9 za barabara zenye kiwango cha lami, kilomita 735.99 zenye kiwango cha changarawe na matengenezo ya kawaida kilomita 430 pamoja na ujenzi wa madaraja 41.
Mikataba 22 iliyosainiwa leo ni sehemu ya Mikataba 32 yenye asilimia 60 ya fedha zote zilitakiwa kutolewa katika mwaka huu wa fedha ambayo ilisainiwa Agosti 14,mwaka huu Mkoani Dodoma.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.