Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance, Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, aliwasili mkoani Njombe tarehe 12 Agosti 2025 kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayofanywa na watumishi wa shirika hilo, sambamba na kutoa elimu ya masuala ya bima. Mara baada ya kuwasili, Bw. Mkeyenge alitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ambapo alieleza dhamira ya NIC kuimarisha utekelezaji wa huduma na manufaa ya bima.Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alimpongeza Bw. Mkeyenge kwa kuchukua hatua za vitendo kwa kutembelea ofisi hizo, akisema kuwa ziara kama hizo huongeza ari na ufanisi wa kazi miongoni mwa watumishi. “Ujio huu wa Mkurugenzi Mtendaji unaonesha uwajibikaji wa hali ya juu na unatoa hamasa kwa watumishi wetu. Shirika la Bima la Taifa limeendelea kuwa nguzo muhimu katika kulinda mali na maisha ya wananchi kupitia huduma zake za bima mbalimbali,” alisema Mhe. Mtaka.Kwa mujibu wa taarifa za NIC, shirika hilo linatoa huduma za bima za aina mbalimbali ikiwemo bima za magari, mali pamoja na kuendesha kampeni za elimu ya bima nchini kote ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wadau wanaohusika na upatikanaji wa huduma za bima.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.