Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga Julai 03, 2024 amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 - 2025 kwa kipindi cha Miaka Mitatu 2021/2022 - 2023 hadi 2024 ambapo Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Mjini Makambako.
Mhe. Deo Sanga amesema kuwa, katika kipindi cha Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Mji Makambako imetekeleza miradi yenye zaidi ya Shilingi ya Bilioni 14 ikiwa ni pamoja na Miradi ya Kada ya Afya, Elimu, Barabara, Maji na Umeme.
Aidha, katika Mkutano huo wa utoaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, amehudhuria Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka.
Wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano huo Mhe. Mtaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa Fedha za Kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Njombe na amempongeza Mbunge wa Jimbo la Makambako kwa kuendelea kuwa karibu na wananchi wa Makambako haswa kuendelea kuufungua mji wa Makambako kwa kutekeleza na kusimamia miradi inayotekelezwa kwa Wananchi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.