Jopo la Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan waliokuwa katika Kambi ya Siku tano mkoani Njombe wakitoa matibabu ya Kibingwa wamehudumia watu zaidi ya 2500 katika Hospitali zote za Wilaya na Halmashauri ndani ya mkoa huo.
Hayo yameelezwa leo tarehe 11 Mei, 2024 na Kaimu Mganga Mkuu wa Njombe, Dkt. David Ntaindwa baada ya hafla fupi ya kuwaaga Madaktari hao katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Amesema, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Njombe waliojitokeza kupata huduma hizo za kibingwa zilizojumuisha, Huduma za Kibingwa za Upasuaji, Magonjwa ya wanawake na Uzazi, Huduma za Kibingwa na Bobezi za watoto, Magonjwa ya Ndani, na wataalamu wa Usingizi na ganzi.
Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika kambi hizo, ili kunufaika na Mpango Kabambe huo ambao umenuia kusogeza huduma za kibingwa na Ubingwa Bobezi karibu na wananchi, pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa mbalimbali katika Ngazi ya Afya ya Msingi.
Jumla ya Halmashauri zote sita (6) za Mkoa wa Njombe zimenufaika na mpango huo, ikijumuisha Halmashauri ya mji Njombe, Makete, Wanging'ombe, Ludewa, Makambako na Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Mwisho.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.