Watoto Elfu Tisa Mia Moja Themanini na Moja wenye umri chini ya miaka Mitano na walio katika ratiba ya chanjo wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya surua, polio na vichomi pamoja na wasichana Mia Nane Thelathini na Tisa wenye umri wa miaka Tisa hadi Kumi na Nne wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mkoani Njombe.
Akizungumzia zoezi hilo Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Mh.Bi. Judica Omar amesema zoezi hilo ni la siku Saba tangu Tarehe Mbili hadi tarehe Nane.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Juma Mfanga amesema zoezi hilo litafanyika katika vituo vya kutolewa huduma za afya, shuleni na nyumbani ili kuwafikia wanawake wajawazito na watoto wote ambao bado hawajapata chanjo hizo na ambao wamepitiliza muda wa kupata chanjo.
Uzinduzi wa zoezi hili unaashiria kuanza kufanyika katika wilaya zote za mkoa wa Njombe ambapo kauli mbiu ni Tuwafikie watoto kwa chanjo na jamii yenye chanjo ni jamii yenye afya
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.