Waziri wa Wizara ya Maji, Mhe. Juma Aweso, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi mkoani Njombe tarehe 22 Julai, 2025, kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya Miji 28. Ziara hiyo inalenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama.
Katika ziara hiyo, Mhe. Aweso atakutana na viongozi wa mkoa, watendaji wa sekta ya maji, pamoja na wananchi wanaonufaika na miradi hiyo ili kupata mrejesho wa moja kwa moja. Ziara hii ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa kote nchini.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.