WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lifanye utafiti wa kina katika vijiji vya Msete na Lugenge ili kujua uwezo wa kasi ya maji yanayozalisha umeme wa maji uliobuniwa na wabunifu John Fuke maarufu Mzee Pwagu na Lainery Ngailo wenye nguvu ya kilovoti 28na kilovoti 15 ili kuwezesha vijiji vingine viweze kunufaika.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani ambaye aliwatembelea wabunifu hao wa umeme wa maji, aliwasifu kutokana na namna walivyoweza kufanikisha kuzalisha umeme huo, lakini akatoa ushauri kwa mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia uzalishaji wa umeme umeme huo unafanywa kwa kuzingatia kisheria za nchi.
Awali mbunifu wa umeme wa maji mkoani hapa John Fute maarufu kwa jina la Pwagu alimweleza Waziri wa Nishati Dk. Kalemani kuwa jamii inayomzunguka imekuwa na shauku kubwa ya kupata umeme anaouzalisha huku changamoto kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundombinu bora na yenye uhakika katika kuwafikishia huduma hiyo.
Aidha katika hatua nyingine akiwa Wilayani Makete, Waziri wa Nishati Mh.Medard Kalemani aliwasha umeme katika shule ya msingi Kiduga iliyopo kata ya Ndulamo pamoja na kituo cha Afya na kuwataka wananchi kuendelea kuweka umeme wa gharama nafuu wa REA Awamu ya Tatu kwa sababu serikali imedhamiria hivi sasa kila mwananchi apate umeme ili kuchochea kasi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mh.Christopher Ole Sendeka amesema wananchi wa mkoa wa Njombe wamenufaika na hatua ya muda mfupi ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano kuhusu upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme,ambayo imewawezesha wananchi kuanzisha na kuviendeleza viwanda vikubwa,vya kati na vidogo vidogo vikiwemo vya kusindika mazao mbalimbali.
Nao baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Regina Mgeni kutoka katika kata ya Ndulamo wilayani makete kwa upande wao hawakusita kutoa pongezi zao pongezi kubwa kwa serikali kuhusu hatua inazozichukua za kuwasogezea huduma ya umeme wa gharama nafuu(REA) katika vijiji wanavyotoka.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.