Waziri wa Kilimo Hussein Bashe jana Januari 17, 2023 alifanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Njombe na kutembelea maghala mbalimbali ya pembejeo za Kilimo.
Mhe. Waziri aliagiza kufungiwa kibali kwa kampuni ya Kandia Fresh pamoja na kutojihusisha na ununuzi na uuzaji wa matunda ya Parachichi ndani na nje ya nchi kutokana na kampuni hiyo kununua Parachichi ambazo hazijakomaa kisha kuzitupa dampo.
Mhe. Bashe alitoa agizo hilo jana mara baada ya kusambaa kwa video iliyoonesha rundo la Parachichi zikiwa zimetupwa mjini njombe.
Waziri Bashe alisema ni marufuku kuchuma Parachichi ambazo hazijakomaa kwa sababu hakuna soko kwa aina hiyo ya parachichi bali ni kuharibu soko la parachichi kimataifa.
Aidha alisema wizara imeandaa muongozo utakaotumika kitaifa kusimamia mnyororo mzima wa uzalishaji wa zao la parachichi.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka walimpokea Mhe. Waziri wa Kilimo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.