Watumishi wa Umma Mkoani Njombe wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Taasisi( PIPMIS )na yale ya Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma( PEPMIS)
Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 20,Novemba hadi 25 Novemba 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, yakiwahusisha Sekretarieti ya Mkoa, Wakarungenzi,Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri na wasaidizi wao.
Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Mipango na Uratibu Ndg. Bruno Mwakipesile kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari,amewataka Watumishi hao kuzingatia mafunzo yanayotolewa kwani yataongeza umakini katika vituo vyao vya kazi wanapowajibika wakati wote na kuendana na mifumo ya utendaji kazi kidigitali. “Nawasihi watumishi mnaopata mafunzo haya ambayo yanafanyika nchi nzima hakikisheni mnatoa ushirikiano katika kuhakikisha tunafikia kusudio la serikali kufikia malengo yaliyowekwa” Amesisitiza Mwakipesile
Kwa Upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi na Umma Utawala bora Bi. Martha Wilimo ametoa maelekezo ya kuhakikisha usimamizi wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma unazingatiwa kwa kufuata vigezo wakati wote na upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa serikali uzingatiwe.
Kuanzia 2023 na kuendelea utendaji kazi utasimamiwa na mifumo ya kielektroniki ya Usimamizi wa Utendaji kazi( PEPMIS na PIPMIS) na mfumo wa Tathmini ya rasilimali watu ili kujiridhisha kama jukumu hilio linatekelezwa ipasavyo.﮴ Katika mifumo hii itatusaidia kubaini hali ya mahitaji ya rasilimali watu,kufanya tathmini ya uhitaji wa Maafisa, wasaidizi na watumishi wanaohitajika ili kupata mahitaji sahihi ya watumishi wanaohitajika kwani mfumo utachakacha wenyewe idadi ya mahitaji ya watumishiwanaohitajika.“
Pia Uwepo wa mfumo huu utakwenda kusaidia upatikanaji wa rasimali watu katika maeneo ya kazi na kusaidia utoaji wa vibali vya Ajira ili kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika Ofisi mbalimbali za Umma. Mfumo huu utahakikisha kabla au ifikapo Disemba 31,2023watumishi wote wawe wamejasijiliwa na kuwezehs watumishi, wakuu wa idara na vitengo kuandaa mipango ya utendaji kazi kabla au ifikapo tarehe husika na kupata taarifa ya mahitaji ya rasilimali watu.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.