Kaimu Katibu Tawala Msaidizi( Uchumi na Uzalishaji) wa Mkoa wa Njombe Bw. Ayoub Mndeme amefungua mafunzo ya mfumo mpya wa manunuzi wa NATIONAL e-PROCUREMENT SYSTEM OF TANZANIA (NeST) kwa wataalam 36 kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe huku akizitaka Taaasisi zote za Serikali kutumia mfumo huu pale tu utakapoanza rasmi kwa sababu Zaidi ya asilimia 70% ya fedha ya Serikali zinatumika katika shughuli za maendeleo kwa kufanya Azinatumika vizuri kwa kutumia mfumo wa manunuzi wa NeST ili kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Aidha wakati akifungua mafunzo haya ameishukuru PPRA kwa kuwezesha mafunzo haya ya mfumo mpya wa NeST ambao unatarajia kuanza tarehe 1 octoba 2023. Pia amesisitiza washiriki wa mafunzo haya, kutekeleza kwa vitendo ili nao wakawe wakufunzi kwenye maeneo yao na kuhakikisha Mkoa na Halmashauri zote zinatumia mfumo huo kikamilifu ili kuepuka Maafisa Masuuli kupigwa faini kwa kushindwa kutumia mfumo huu.
Mndeme amesema kuwa matumizi ya Mfumo huo mpya, taratibu zote za manunuzi zitafanywa kwenye Mfumo ikiwa na maana kuanzia uandaaji wa mahitaji ya Idara, Uanzishaji wa Tenda, Uthamini, Utoaji wa Tenda na Majadiliano,
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.