Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica OmarI amesema jumla ya watu 311 Wenye Ulemavu katika Vikundi 197 wamenufaika na Mkopo wa asilimia mbili unaotolewa na serikali Kwa ajili ya Kuendesha shughuli kujikwamua kiuchumi.
Amesema hayo 23 Novemba, 2023 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Ugemaji wa Rasilimali kwa Watu Wasioona lililofanyika katika ukumbi wa Agreement Mkoani humo.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi imehakikisha kundi hilo linathaminiwa na kushirikishwa katika fursa za kiuchumi na kuwajengea mazingira wezeshi ili waweze kushiriki katika kila fursa zinapotolewa.
Akizungumza katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Rasheed Maftaa amesema kongamano hilo lililenga kutoa mafunzo, kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Utunzaji wa rasilimali zinazowasaidia katika uendeshaji wa vyama vyao.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wasioona Seleman Idrisa, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kendelea kuwapa kipaumbele watu hao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.