Wananchi 796 Wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi katika mkoa wa Njombe wamehudumiwa bure na mawakili wa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia Septemba 19 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho wakati wa hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya miaka 27 ya kituo hicho, ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya migogoro hiyo ni ile ya ardhi ambayo ni 384.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa migogoro mingine ni ile ya ndoa na kutelekeza watoto 109, Mirathi 57, ajira na kazi 46, Madai 47 na kesi za jinai 39 huku akibainisha sababu za migogoro ya ardhi kuwa ni uuzaji holela wa maeneo.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary amekiri kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi katika mkoa na kueleza kuwa serikali itakuja na mpango wa kupima na kurasimisha maeneo yote ya wananchi ili kuepukana na migogoro hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Mary Makondo amesema wizara imekusudia kufanyia maboresho kwa baadhi ya sheria ili kurahisisha utatuzi wa migogoro mbalimbali kwa wakati.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.