Wananchi katika Halmashauri nya Mji wa Njombe wametakiwa kujiunga na Bima ya Afya Iliyo boreshwa ili waweze kutibiwa bila kupata usumbufu wowote pindi watakapo kumbwa na magonjwa na hivyo kujihakikishia kupata huduma za Afya kwa uhakikia zaidi pindi watakapofikwa na dharura.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mh. Ruth Msafiri wakati wa uzinduzi wa CHF iliyoboreshwa katika kituo cha Afya Njombe Mjini ambapo amesema kuwa kuna faida nyingi za kujiunga na CHF hiyo ikiwemo kuhudumia watu sita katika kaya.
Amesema faida nyingine ni pamoja na kutibiwa pasipokuwa na gharama yeyote mara baada ya kupata kadi ya CHF inayogharimu Shilingi 30,000 na Hivyo kuwahamasisha wananchi kuichangamkia CHF iliyoboresha.
Aidha Mkuu wa Wilaya amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe kupita katika Eneo lake la Kiutawala na Kuangalia ni kwa nini ombaomba wameongezeka katika Halmashauri yake ili kubaini changamoto za watu hao zitatuliwe ikiwezekana kama wanachangamoto kubwa ya kuhudumiwa basi halmashauri ichukue jukumu hilo la kuwalipia CHF iliyoboreshwa na wao kuwa sehemu ya wanufaika.
Kwa upande wake Mariam Monjesa ambaye ni Mratibu wa CHF kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe amesema kuwa bado kumekuwa na mwitikio mdogo wa watu kujitokeza kupata huduma hiyo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.