Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh.Dkt Philip Isdor Mpango, amesema serikali imepanga kujenga uwanja mkubwa wa ndege Mkoani Njombe. Ameyasema hayo wakati akihitimisha maonyesho ya nne ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogo( SIDO) yanayofanyika kitaifa Mkoani Njombe.
Makamu wa Rais amesema Serikali imedhamilia kufanya ujenzi mkubwa wa kiwanja cha ndege utakaohusisha ujenzi njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilometa Tatu ,Jengo kubwa la abiria na jengo maalumu kwa ajili ya kuhifadhia bidhaa zinazoharibika haraka.
Pia amesema Serikali inatambua fulsa mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kilimo cha Parachichi,Viazi, Ngano na umuhimu wa usafiri na usafirishaji hivyo serikali imeamua kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa ndege Mkoani Njombe.
“Sisi Serikali tunaamini uwepo wa usafiri wa uhakika utachangia kuinua na kukuza uzaluishaji viwandani na mashambani lakini pia kuinua sekta ya utalii Mkoani Njombe”Alisema Mheshimiwa Mpango
Uwanja wa ndege utakao jengwa mkoani Njombe utakuwa na uwezo kupokea ndege kubwa za abiria Pamoja na ndege za mizigo.
Naye Mkuu wa Mkoa Mh. Antony Mtaka amaetumia wasaha huo kuwakaribisha watanzania wote wanaohitaji kufuga ngo’mbe wa maziwa wafike katika shamba la ngo’mbe la Kitulo lilipo wilaya ya Makete Mkoani Njombe Kununua Mitamba hiyo.
Mtaka ameyasema hayo wakati akikabidhi zawadi ya Mkoa kwa MhMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango,aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye kilele cha maonyesho ya viwanda vidogo SIDO yaliyofanyika kitaifa Mkoani Njombe.
‟Mheshimiwa Makamu Rais, kuna wakati wafugaji walilazimika Kwenda mpaka Afrika Kusini kununua Ngo’mbe bora kutokana na shamba letu kuyumba ,tunaamini kwa zawadi hii wewe mwenyewe utakuwa shahidi kwenye uzalishaji wa maziwa” Alisema Mh.Mtaka.
Pia Katibu Tawala Mkoa wa Njombe amekabidhi Kamba za kufungia Ngombe na Mkoa utaratibu usafirishaji wa ngo’mbe hao hadi kufika nyumbani kwa Mh.Dkt. Mpango.
Sambamba na zawadi hiyo Halmashauri ya Mji Njombe Ikiwakilishwa na Mwenyekiti wako Mh.Erasto Mpete amemkabidhi hati ya kiwanja,Pamoja na miche ya karanga aina ya Makademia.
Baada ya kukabidhiwa zawadi hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais, ametoa shukrani kwa namna Mkoa wa Njombe ulivyomkarimu kipindi chote alichofanya ziara Mkoani humo,naahid kurudi tena Njombe kutembelea maeneo ambayo sijafika.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.