Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ametoa rai kwa Watanzania kupenda na kunununua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda nchini ili kupanua wigo wa masoko ya bidhaa, kuongeza uzalishaji kukuza viwanda, kuongeza ajira na kipato cha mtu binafsi na pato la Taifa. Kigahe ameyasema hayo Oktoba 23, 2023 alipokuwa akifungua Maonesho ya nne (4) ya Shirika Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba Mkoani Njombe kuanzia 21 - 31/ 10/2023 yakiongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Pamoja Tujenge Viwanda kwa Uchumi na Ajira Endelevu”.
"Niwahakikishie kuwa iwapo tutaunganisha kilimo na viwanda tutaweza kukuza soko la ndani lakini pia kupunguza uagizaji bidhaa ambazo tunaweza kuzizalisha sisi wenyewe kutokana na mazao ya kilimo na malighafi nyingine ambazo tunaweza kuzalisha ndani,lakini zaidi tutaweza kuingiza bidhaa zetu katika masoko ya nje na ya kimataifa"alisema Kigahe.
Alifafanua kuwa"Kwanza nyinyi ni mashahidi tunamasoko ya kikanda jumuia ya afrika mashariki bado hatujaitumia ipasavyo lakini jumuia ya maendeleo kusini afrika SADC bado hatujatumia soko lake vema, lakini zaidi sasa tunaeneo huru la biashara Afrika na huko kuna masoko mengi ya bidhaa nyingi na hasa zinazotokana na bidhaa zinazoongezwa thamani na mzao ya kilimo"alisema.
Kigahe alisema serikali imejipanga kuhakikisha inalisha dunia na afrika kwa bidhaa ambazo zimeongezwa thamani."Sio kuuza nje Parachichi kama ilivyo,kuuza Mahindi kama yalivyo,Alizeti na mengineyo,tuuze unga,tuuze bidhaa zilizoongezwa thamani,tuwalishe chakula ambacho kimeongezwa thamani kutoka Tanzania"alisema Kigahe.
Aidha amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO kushirikiana na Halmashauri ili kuhakikisha vijana wanapata teknolojia ili kuweza kifanya kilimo kibiashara. Katika hatua nyingine, ameishauri SIDO kuendelea kuratibu Maonesho hayo Kitaifa kufanyika Mkoani Njombe kila mwaka kama ilivyo vya Sabasaba kitaifa kila mwaka ni Dar es Salaam , Dhahabu ni Geita kwa kuwa Maonesho hayo yanaonyesha taswira nzima ya bidhaa za kitanzania teknolojia, ubunifu,Mafanikio ma fursa kwa Mtanzania kutumia na kupanua wigo wa Uzalishaji.
Meneja mahusiano mwandamizi huduma za benki kwa serikali NMB Josephine kulwa,alisema maonesho hayo ni fursa kwa wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara mkoani Njombe ili kupata elimu ya mambo mbalimbali ikiwemo huduma zinazotolewa na benki ya NMB.
"Lengo la kudhamini kuhamasisha maonesho haya ni kutoa fursa kwa wajasiriamali,wakulima,wafanyabishara waweze kufahamu uwepo wa maonesho haya,benki ya NMB ambacho tumekuja nacho hapa kwanza tunatoa elimu ya ujasiriamali,tunatoa elimu ya kufedha na kukuwezesha kuona jinsi gani unaweza kukopesheka na mabenki mbali mbali hasa kwa upande wa benki ya NMB tunafanya mikopo mbalimbali kwa wajasiriamali ikiwemo mkopo wa mshiko fasta"alisema Josephine.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku kwenye mbolea ili kuongeza uzalishaji kwenye mazao ya chakula.
"Kwa sababu kwa kutoa kwake ruzuku imetusaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na uzalishaji wa mazao ya kibiashara hivyo naamini maonesho haya yatatusaidia teknolojia ndogondogo ambazo zitatusaidia kuchagiza uzalishaji katika katika mkoa wa Njombe"alisema Kissa.
Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mhandisi Prof.Sylivester Mpanduji,alisema wamejipanga kutoa elimu kupitia simu za mkononi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao watahamasika kuanzisha viwanda.
Vilevile, ameielekelza Wakala wa Maendelo ya Viwanda Vidogo na vya Kati.(SMIDA) kushirikiana na SIDO katika kupata teknolojia na kuwawezesha vijana wa Zanzibar kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji ili nao waweze kuitumia fursa ya uwepo wa AFCFTA, EAC, SADC, AGOA na fursa nyingine za masoko ya pamoja.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.