Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia kifungu cha sheria ya watu wenye ulemavu na 9 ya mwaka 2010 inayomtaka kila mwajiri aliyeajiri kuanzia watu 20 kuhakikisha asilimia 3 ya waajiri wake ni watu wenye ulemavu.
Agizo hilo limetolewa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira,Vijana na Watu Wenye Ulemavu prof.Joyce Ndalichako wakati wa maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe kitaifa Mkoani Njombe.
Alisema serikali inachukua juhudi mbalimbali katika kuimarisha ustawi wa watu wenye ulemavu hususani upande wa Elimu,Afya,Miundombinu,Ajira pamoja na ushiriki kwenye nafasi katika jamii.
“Nawapongeza pia kwa kutambua juhudi za serikali katika kushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu ikiwemo kwa kuendelea kuwaajiri watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona,”alisema Ndalichako.
Alisema serikali imekuwa kinara katika kuthamini watu wenye uleamavu sambamba na kuboresha miundombinu ya shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum.
‘’Mwaka jana disemba 2022 mama yetu Mh Dk.Samia Suluhu Hassan alielekeza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za miaka 61 ya uhuru shilingi milioni 960 kutumika kujenga mabweni katika shule 8 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo wasioona,”alisema Ndalichako.
Ndalichako alisema serikali ya awamu ya sita kwa mwaka wa fedha 2022/23 imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili kujenga vyuo vipya katika Mikoa ya Kigoma,Ruvuma na Songwe,vile vile kwa kushirikiana na wadau imetolewa takribani shilingi milioni 500 kujenga chuo kipya kisesa Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLD), Omari Mpondelwa alisema watu wasioona ni watu kama watu wengine hivyo jamii isiwanyanyapae.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh. Antony Mtaka alitoa rai kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum mkoani humo kuwaacha watoto waende shule.
“Tunapoandikisha darasa la kwanza waacheni watoto waje shule na kama kuna mtoto anachangamoto,afisa elimu yupo mwambie mtoto wangu anachangamoto kuangalia namna ya umsaidia mtoto kwenye shule nyingine,’’alisema Mtaka.
Mtaka alisema kuwa serikali ina mfumo mzuri wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum kwa uwepo wa vyuo,walimu pamoja na vifaa.
Akisoma risala Kaimu Katibu Mkuu Taifa kutoka Chama cha Watu Wasioona(TLD)Subira Shedangio alisema chama hicho kilianzishwa kutokana na madhila wanayokutana nayo ya kunyanyaswa kubaguliwa.
Alisema Chama kinamuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuona umuhimu wa kukipatia chama hicho ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali.
Shedangio alitaja changamoto kuwa ni gharama za bima za afya kuwa kubwa kwa watu wasiiona kwa sababu hakuna kipato cha uhakika.
“Kwa sasa kuna mabadiliko ya utoaji wa bima za afya mfano watoto waliopo shuleni kuwa na idadi maalum ambapo watoto wasioona wanaosoma katika shule za bweni na vitengo ambao hawawezi kutimia idadi hiyo kukosa huduma,”alisema Shedangio.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.