Serikali imesema iko mbioni kukamilisha mazungumzo na mwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe kwa kuzingatia sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu mkataba yenye masharti hasi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la mradi huo, amesema mazungumzo hayo yanakwenda sambamba na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuongeza pato la taifa na kuleta maendeleo.
“Sasa ni dhamira ya dhati kabisa ya kusema kwamba mradi unakwenda kuanza tunayo malengo kwenye Ilani yetu ya chama ya mapinduzi lakini pia katika maono yetu ya 2025 tumeeleza wazi huu ni mradi muhimu,” alisema Dk. Chana.
Waziri Dkt. Chana alisema kuwa watanzania wanayo kiu ya kuona kwamba mradi huo wa kimkakati wa liganga na mchuchuma unaanza mara moja.
“Sisi kama wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na Biashara waziri mwenzangu anayesimamia masuala la viwanda tunaendelea kusimamia suala hili kwa karibu sana,” alisema waziri Dk. Chana.
Pia Dkt. Chana alibainisha kwamba, “Na tunataka miradi hii ya mchuchuma na liganga iwanufaishe watanzania wote kama jinsi ambavyo sheria zetu tulizopitisha mwaka 2017 zinavyosema mali asili za taifa, mali asilia zinapaswa kutumika kwa manufaa na faida ya watanzania wote,” alisema.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uangalizi na Utajiri wa Rasilimali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Neema Mwanga alisema mchakato wa mradi huo upo kwenye mazungumzo ili kupitia sheria za mikataba.
“Mnamo mwaka 2017 Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria mbili, sheria ya mamlaka ya nchi kuhusu umiliki wa utajiri na maliasili za nchi na sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu mikataba yenye masharti hasi,” alisema Mwanga.
Mwanga anafafanua kuwa, “Sheria hii ya pili inataka mikataba yote inayoingiwa na wawekezaji katika uchimbaji au uvunaji na matumizi ya utajiri na mali asili za nchi ulenge katika kuhakikisha rasilimali zinapatikana, kuongeza pato la taifa lakini kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi,” alisema.
Aidha alisema kuwa kwa sababu nchi inahitaji wawekezaji, hivyo ni lazima mikataba inayoingiwa iwe na tija kwa sababu sheria zimesisitiza.
Meneja Mradi wa Liganga na Mchuchuma kutoka Shirika la Taifa la Mendeleo (NDC) Dk. Witness Ishuza alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika katika eneo la liganga kuna tani zaidi ya milioni 128 za chuma.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.