Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni ameagiza wakuu wa shule na maafisa elimu katika wilaya hiyo kuwasimamia wasaidizi wao (walimu) wasiweze kutoroka kwenye vituo vyao vya kazi wakati wa muda wa muajiri wao na kwenda kutafuta fedha za kujiongezea vipato kwa kuwa serikali imeshatoa fedha kwa ajili yao.
Ametoa agizo hilo wakati akizindua vitabu vya mwongozo wa kufundishia na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi ambapo amesema kuwa Bado kuna changamoto ya utoro kwa wanafunzi na walimu.
“Sio utoro tu kwa wanafunzi upo utoro na kwa walimu kwa hiyo maafisa elimu,wakuu wa shule mkawasimamie wasaidizi wetu wasitoroke watimize dajibu wao,sasa hivi serikali imeshamwaga mahela tena wala sio ya UVIKO ila ni ya kwetu sisi wenyewe”amesema Kanoni
Vile vile ameelekeza shule zilizopewa jukumu la kujenga madarasa ziweze kuanza kufanya maandalizi ya kutosha kwa kuwa tayari serikali imetoa siku 75 kwa wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi.
Vile vile ameelekeza shule zilizopewa jukumu la kujenga madarasa ziweze kuanza kufanya maandalizi ya kutosha kwa kuwa tayari serikali imetoa siku 75 kwa wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi.
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Lauteri Kanoni akizungumza na Mwalimu pamoja na wanafunzi katika ukumbi wa halmashauri hiyo wakati akizindua vitabu vya mwongozo wa kufundishia na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.