WATUMISHI wa sekta ya madini mkoani Njombe wametakiwa kukusanya Mapato kwa weredi mkubwa sambamba na kuridhika kwa kile wanachopewa.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi Judica Omari alipowatembea na kuzungumza na watumishi wa sekta ya madini Mkoani Njombe.
‘’Nasisitiza umuhimu wa kuwahi kazini na nachukia mtumishi anayeidharau kazi yake kwa sababu hiyo kazi ndo unakufanya uonekane ni mtumishi japo kipato ni kidogo anachokipata kinamsaidia kukidhi mahitaji yake,’’amesema Bi.Judica.
Bi Judica amezitaka ofisi kujitahidi kuendana na teknolojia za kisasa za kutumia mfumo wa computer,computea Mpakato na kuachana na teknolojia ya makaratasi.
Christina Mzena akimuwakilisha Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu,amewakumbusha watumishi kuhusu uwajibikaji na maadili ya kazini na kuepuka rushwa.
Naye Meneja wa Madini Mkoa Bi.Zabibu Napacho amemshukuru na kumpongeza kwa niaba ya watumishi wenzake Katibu Tawala Bi. Judica Omari kwa kusikiliza changamoto mbalimbali ikiwemo za kisekta na tunakuahidi kuipeleka mbele sekta madini.
‘’Sisi kama sisi hatuwezi Kwenda mbele bila kuwa na mtu wa tatu ambaye ni mchimbaji na yeye unakuta changamoto yake ni mtaji,hivyo tutawakaribisha wachimbaji kuja Njombe kuwekeza,’’amesema Zabibu.
Kwa upande wake Injinia. Fredrick Girenga ameushukuru uongozi wa mkoa katika harakati za kuleta maendeleo kupitia madini amabyo yatafungua uchumi na kupatikana kwa fursa zitakazotokana na madini.
‘’Mpaka sasa ni leseni 40 ndizo zinazofanya kazi kati ya leseni 300,ombi kwa serikali ni wachimbaji wadogo wapewe eneo ili waweze kuchimba kwa urahisi ,wachimbaji wengi wanaoweza kuchimba changamoto ni soko,’’amesema Girenga.
Pia amesema kumekuwa na changamoto ya watu kupitisha madini ya ujenzi kwa mgongo wa serikali kwa lengo la kukwepa kulipa ushuru kwenye vituo vya ukaguzi.
Pia sekta ya madini mkoani Njombe wameishukuru serikali kwa kulipa fidia kwa wanufaika jumla ya sh.Bil 15.5 na inategemea fedha hiyo kurud tena serikali baada ya kazi kuanza.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.