Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ameagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanafikia asilimia 50 kila Halmashauri na wilaya zilizolengwa ifikapo mwaka 2020 lengo la wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa unamnufaisha mwananchi.
Ole Sendeka akizundua rasmi maboresho hayo maboresho ya mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF) mkoani Njombe alionyesha kutoridhishwa na kasi ya wananchi kuwa na mwamko wa kujiunga na CHF licha ya serikali kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu hadi ngazi ya hospitali ya rufaa na kutoa wito kwa wananchi kujiunga na mfuko huo ambao utahudumia watu sita kwa kila kaya.
Aidha Ole Sendeka amesema Rais Dk. John Magufuli ataendelea kupongezwa na wananchi wa mkoa wa Njombe kwa hatua yake ya kuwezesha fedha zilizopelekwa kwenye sekta ya afya kiasi cha shilingi bilioni sita ambazo ni zakuongezea kusukuma ujenzi wa hospitali za wilaya pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa iliyopo Wikichi mkoani hapa.
Naye Rajabu Msigwa ambaye ni shekhe wa mkoa wa Njombe anasema maboresho ya mfuko wa Afya ya Jamii yamekuja wakati mwafaka kwa wananchi wa mkoa wa Njombe hasa ikizingatiwa serikali imefanikisha kujenga hospitali ya Rufaa ya mkoa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.