Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh., Christopher Ole Sendeka amewaongezea muda Wadaiwa Sugu wa iliyokuwa Benki ya Wananchi Njombe (Njocoba) kulipa madeni yao.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkuu wa mkoa amesema pamoja na wiki mbili alizotoa kwa wadeni kuanzia terehe 23/10/2019 hadi 7/11/2019, ameamua kuongeza muda hadi tarehe 30 Novemba,mwaka huu ili kuwapa fursa Wadaiwa hao kukamilisha madeni yao.
Akitoa mrejesho wa kikosi Kazi, alichokiunda Oktoba 23, mwaka huu, kukusanya madeni ya Njocoba, Ole Sendeka amesema jumla ya shilingi Milioni 300 zimekusanywa katika kipindi cha siku 14 ambao wadaiwa 71 wamekamilisha madeni yao huku 49 wakiingia mkataba wakulipa madeni yao huku 49 wakiingia mkataba wa kulipa madeni yao kwa kikosi Kazi.
Aidha Ole Sendeka amesema Wadaiwa 216 hadi sasa hawajajitokeza kulipa madeni yao.
Kwa mujibu wa kikosi kazi kilichoundwa Benki ya njocoba ilikuwa na Wadaiwa takribani 336 ambapo madeni ya Benki hiyo yalikuwa takribani shilingi bilioni 1.4.
Benki ya Njocoba iliwekwa chini ya mufilisi wa Benki Kuu ya Tanzania Januari 1, mwaka 2018.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.