Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Prof. Rwekaza Mukandala, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa majengo ya Kampasi ya UDOM katika Mkoa wa Njombe. Wageni hao walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Mtaka alieleza kuwa ujio wa viongozi hao ni hatua muhimu katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuimarisha elimu ya juu nchini. Alisisitiza kuwa ujenzi wa Kampasi ya UDOM mkoani Njombe utafungua fursa pana za maendeleo ya elimu na kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.