NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO MH.JULIANA SHONZA AMEUAGIZA MKOA WA NJOMBE KUJENGA KITUO CHA KUKUSANYIA TAARIFA SAHIHI ZIHUSUZO UTALII NA UTAMADUNI.
Serikali imeagiza kujengwa kwa kituo maalum kitakachowezesha kupatikana kwa taarifa sahihi za utalii na Utamaduni katika mkoa wa Njombe zinazohusu vivutio vya utalii wa utamaduni ikiwemo msitu wa Nyumbanitu unaopatikana kuku weusi wasiofugwa na mtu yeyote na Uwepo wa Jiwe lenye ramani ya Bara la Afrika.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo mh.Juliana Shonza wkati akiwa ziara ya kutembelea msitu wa asili wa Nyumbanitu na jiwe lenye ramani ya Afrika ikiwa ni vivutio vya utalii vilivyopo katika Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani Njombe na kusisitiza ni vyema uongozi wa mkoa ukakuza utalii na utamaduni kupitia vivutio hivyo.
Aidha mh.shonza ameongeza kusema kuwa kwa sasa wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii wanazitambua na kuzibainisha fursa za vivutio vipya vya utalii vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini ili kutoa fursa pana kwa watalii kutembelea na kujionea majaabu ya maeneo hayo hususani msitu wa nyumbanitu.
Awali Mh.Naibu waziri akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa serikali wa wilaya ya wanging’ombe na mkoa wa Njombe kabla ya kuingia ndani ya msitu huo na kupata bahati ya kuwaona kuku weusi ndani ya msitu baadhi ya wazee wanaohusika kuutunza msitu huo akiwemo mzee Elias Mkongwa ambaye ni Chifu wa Wabena amemweleza Naibu waziri shonza kuhusu historia ya msitu na baadae kupata maelezo ya jiwe lenye ramani ya Afrika lililopo katika kijiji cha Igodivaha Kata ya Imalinyi mkoani hapa kuhusu mkakati walionao wa kutangaza vivutio hivyo..
Nae Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe Komredi Ali Kasinge amesema Serikali imejipanga kuendelea kutangaza vivutio hivyo ili kukuza utalii wa ndani katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kupitia maajabu ya msitu wa Nyumbanitu na mapango yake pamoja na jiwe la ramani ya afrika.
kwa upande wao baadhi ya wazee akiwemo mzee Juma Masamaki ambao wanaoutunza msitu wa nyumbanitu na jiwe lenye ramani ya bara la afrika wamemwomba mh.Naibu waziri kuhakikisha miundombinu ya barabara na huduma nyinginezo za kibinadamu zinapatikana katika eneo hilo lenye vivutio hivyo vya utalii ili kujenga hamasa kwa watu mbalimbali kuweza kufika na kujionea maajabu mbalimbali.
mwisho.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.