Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amekuwa Waziri pekee wa kwanza kufika katika Kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na kufurahishwa na namna wananchi walivyoamua kukusanya nguvu zao na kufanikisha ujenzi wa Kituo cha Afya ambacho kitasaidia kuwaepusha na adha ya kutembea umbali wa kilomita 90 kufuata huduma za afya mkoani Njombe.
Naibu Waziri Mwita Waitara ambaye yupo mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi ya kuzitembelea wilaya za Ludewa,Njombe na Makete mkoani Njombe amefanya ukaguzi katika miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali na vituo vya afya na kuahidi serikali itaharakisha inapeleka vifaa tiba na waganaga haraka katika kituo cha Afya Makowo…
Aidha akiwa katika shule ya Msingi Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye uhitaji maalum na kisha kuzungumza na wanafunzi ambapo amesema kama kuna changamoto ya ukosefu wa maeneo ya kujenga madarasa kwenye shule ni vyema yakajengwa madarasa kwa mfumo wa ghorofa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh.Chritopher Ole Sendeka amemhakikishia Naibu Waziri Waitara kuwa kwa mkoa wa Njombe umefanikiwa kuondoa upungufu wa madawati na kwamba mpaka sasa hakuna mwanafunzi anayekaa chini katika shule zote za msingi na sekondari.
Mh,Sendeka ameongeza kuwa katika hatua nyingine mkoa umefanikiwa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari,ili kuhakikisha wanafunzi wanajengewa mazingira bora ya usikivu wakiwa darasani.
“Ili Nchi tuweze kufikia malengo ya kuwekeza katika viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,ni lazima tuwekeze katika sekta ya elimu kwanza kwa lengo la kuwapata wataalamu na kwa kuanzia mkoa wa njombe tumejikita hapo.
Naye Diwani wa Kata ya Makowo, Honoratus Mgaya ameipongeza serikali kwa kusikia kilio chao cha kuwaomba viongozi wa Serikali waweze kufika kwenye kata hiyo kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika hospitali binafsi ya ikonda…
Nao wanafunzi wa shule ya Msingi Kambarage akiwemo Rehema Mgaya kwa upande wao waliomba serikali kuangalia kwa jicho la tatu kwa watoto wenye uhitaji maalum waweze kusaidiwa kupata vifaa vya kusomea…
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.