Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mh. Deogratias Ndejembi,amegiza kufanyika kwa ujenzi usiku na mchana kwenye shule ya sekondari mpya inayojengwa kijiji cha Mbugani kata ya Kitandililo halmashauri ya Mji makambako mkoani Njombe yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 500 kupitia mradi wa SEQUIP.
Ndejembi alilitoa agizo hilo jana mara baada ya kutembelea ujenzi huo na kubaini kususua ambapo alisema mafundi wanapaswa kuongezwa ili majengo hayo yakamilike kwa muda unaotakiwa.
"Nchi nzima mwisho ni tarehe 31 mwezi wa 10 mwaka huu sitabadilisha,hawa mafundi wamebana hela hawaweki nguvu ya kutosha ya kufanya kazi,tuko nyuma na deadline na iko palepale ya tarehe 31,nitarudi hapa tena bila ya hodi kuja kuona ujenzi unaendeleaje na hatua kubwa imefikiwa kumebadilika"alisema Ndejembi.
Aliongeza kuwa"kiukweli tunaenda taratibu tunamuangusha Rais wetu,tunamuangusha mbunge wetu ambaye tena yeye ndio mshika ilani ambayo haya yote yanayofanywa ni katika ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi,hapa hata choo hakijaanza kujengwa hivi tunavyozungumza na fundi mwenyewe site hayupo aliyepewa choo"alisema Ndejembi.
Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu)Dk Charles Msonde,aliahidi kufuatilia maendelea ya ujenzi wa shule hizo mpya nchi nzima ili kuhakikisha octoba 31 mwaka huu,shule zote za SEQUIP ziwe zimekwisha.
"Maelekezo haya umeshatoa tukiwa Dodoma hapa unayasisitiza tu na ndio maana umesita kuongeza hata siku moja na ni maelekezo najua ya mh waziri wa nchi,kwa hiyo wenzangu mafundi waongezwe kazi za sambamba usiku na mchana ili shule hizi zikamilike watoto wasiende kusoma umbali mrefu"alisema Msonde.
Awali mbunge wa jimbo la Makambako ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga,na Diwani wa kata ya Kitandililo Iman Fute walikiri mapungufu na walimuomba naibu waziri kuwaongezea muda.
"Naomba tuwe wakweli kabisa nikuombe kwamba kwamba tutakamilisha ifikapo tarehe 31 mwezi wa 10 tusikudanganye lakini nikuahidi kwamba haitavuka tarehe 20 ya mwezi wa 11 mambo yatakua yamekamilika kabisa,tuombe hizo wiki tatu za extension kwa maana ya kwamba tutapiga kazi kwa kushirikia na usiku na mchana tuhakikishe mambo yanakaa vizuri kama mlivyotukuta mh naibu waziri hatutoki"alisema Fute.
Akisoma taarifa mkuu wa shule ya sekondari Kitandililo Albert Kahonga,alisema serikali imetoa kiasi cha zaidi ya sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ili kuwaondolea wanafunzi changamoto ya kutembea umbali mrefu.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.