Na. Chrispin Kalinga - Njombe
Ikiwa ni siku ya pili tangu Mwenge wa Uhuru 2024 uanze kukimbizwa Mkoani Njombe Juni 17, 2024 Umeanza kuiangazia miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa Katika kata ya Matola ,Kijiji cha Boimanda.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Mji Njombe umepitia miradi 6 na shughuli 2 ,shughuli 1 ikiwa ni ukaguzi wa klabu ya kupambana na Rushwa na Shughuli nyingine ni uzinduzi wa wimbo wa uhamasishaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kwa upande wa miradi Mwenge wa Uhuru umezindua miradi 3 na kukagua miradi 3.
Katika kata ya Matola Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba 3 vya Madarasa ya Shule ya Msingi boimanda na Ofisi 1 ya Walimu vyenye thamani ya jumla ya shilingi 97,050,552.00
Ukiwa kata ya Uwemba Mwenge wa Uhuru Umekagua Msitu wa asili wa Isililo wenye ukubwa wa hekta 58.8 na thamani ya shilingi 189,229,000.00
Ukiwa kata ya Yakobi Mwenge wa Uhuru umekagua shamba la parachichi la mwekezaji Frank Msuya lenye ukubwa wa ekari 200 ambalo uwekezaji wake ni shilingi billioni 1.
Katika kata ya Mjimwema Mwenge wa Uhuru umefanya uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Amoil ambacho uwekezaji wake ni zaidi ya millioni 721,083,707.00 na kata ya Njombe Mjini Mwenge wa Uhuru umefanya Ukaguzi wa kikundi cha vijana cha Sungura Njombe (SUNJO) ambao ni wanufaika wa mikopo inayotolewa na Halmashauri ambacho mpaka sasa kikundi kimefikia thamani ya shilingi millioni 30.
Na katika kata ya Ramadhani Mwenge wa Uhuru Umezindua jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena) ambalo limejengwa kwa shilingi milioni 173 ,167,000.00
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 inasema "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.