Mwenge wa Uhuru 2025 umeingia rasmi mkoani Njombe ukitokea mkoani Iringa, ambapo Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, ameupokea kwa niaba ya wananchi wote wa Njombe. Hafla hiyo ya mapokezi imefanyika katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi waliokusanyika kwa wingi kuonesha uzalendo wao.
Tukio hili limeashiria kuanza kwa mbio za Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Njombe, ambapo mwenge huo utapita katika wilaya zote ukikagua, kuzindua, na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo. Mbio hizi huchochea uwajibikaji, ushiriki wa wananchi na kuchangia maendeleo endelevu katika jamii
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.