MKUU WA MKOA WA NJOMBE,MH.CHRISTOPHER OLE SENDEKA AMEAMURU KAIMU MHANDISI WA MAJI WILAYA YA MAKETE MKOANI NJOMBE,DANIEL SANGA KUSHIKILIWA NA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NA JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE, KWA HATUA ZA KISHERIA,MARA BAADA YA KUTUHUMIWA KUTENDA KOSA LA KUGHUSHI NYARAKA ZA HALMASHAURI HIYO KWA LENGO LA KUTOA UPENDELEO KWA MMOJA WA WAOMBAJI WA ZABUNI YA KUJENGA MRADI WA MAJI WILAYANI HUMO.
MH.SENDEKA LICHA YA KUCHUKUA HATUA HIYO PIA AMEIONYA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO YA HALMASHAURI HIYO,KWAMBA HAITABAKI SALAMA KUTOKANA NA KUSHINDWA KUZINGATIA NA KUSIMAMIA SHERIA ZA MANUNUZI NA KULAZIMIKA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI(CAG),KUIBUA HOJA ZILIZOPELEKEA HARUFU YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA KUISABABISHIA HASARA HALMASHAURI HIYO.
AIDHA KATIKA KIKAO HICHO CHA BARAZA MAALUM LA MADIWANI LA KUPITIA HOJA ZA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE KIMEFANYIKA WAKATI HALMASHAURI HIYO IKIWA IMEPATA HATI YENYE MASHAKA,JAMBO AMBALO MKUU WA WILAYA HIYO VERONIKA KESSY AMELAZIMIKA KUANISHA MOJA YA SABABU ZILIZOPELEKEA KUPATA HATI HIYO NI KUTOKANA ANA KUTOKUWEPO KWA USHIRIKIANO KATIKA BAADHI YA IDARA MBALIMBALI NA KWAMBA WATUMISHI WA UMMA WATAKAOBAINIKA KUFANYA NDIVYO SIVYO KWENYE FEDHA ZA UMMA HATUA KALI ZITACHUKULIWA…
TAARIFA ZA AWALI ZINAONYESHA KUWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE IMEPATA HATI YA MASHAKA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 HII NI KUTOKANA NA WATUMISHI WA IDAYA YA FEDHA NA MANUNUZI KUKIUKA TARATIBU ZA MANUNUZI NA FEDHA JAMBO AMBALO BAADHI YA WATUMISHI HAO AKIWEMO DANIEL SANGA AMBAE NI KAIMU MHANDISI WA MAJI ANAETUHUMIWA KWA KUGHUSHI NYARAKA AKALAZIMIKA KUTOA UTETEZI MBELE YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE MH.CHRISTOPHER OLE SENDEKA,KWA KUSEMA KUWA BODI YA TATHIMINI YA ZABUNI YA HALMASHAURI HIYO ILIRIDHIA MCHAKATO WA MANUNUZI NA UTEUZI WA MKANDARASI WA KUJENGA MRADI WA MAJI,JAMBO AMBALO SIYO KWELI.
KATIKA KIKAO HICHO MARA KADHAA KILILAZIMIKA KUSIMAMA KWA MASAA KADHAA HII NI KUTOKANA NA KILE KILICHODAIWA BAADHI YA WATUMISHI KUTOWASILISHA NYARAKA MUHIMU ZA TAARIFA ZA IDARA ZAO JAMBO AMBALO KATIBU TAWALA WA MKOA WA NJOMBE,CHARLES KICHERE ALILAZIMIKA MARA KADHAA KUTOA MAELEZO YA KUHOJI JUU YA USAHIHI NA UMAKINI WA TAARIFA ZA WATAALAMU HAO,
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.