Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amemashukuru Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko kwa kufanya ziara ya kikazi ndani ya mkoa wa njombe kwa siku 2 iliyoanza tarehe 21 Februari 2024 na kumalizika leo tarehe 22 Februari 2024.
Wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Makete mara baada ya kukagua eneo linatarajiwa kujengwa Bwawa la Kufua umeme, katika Kijiji cha Madihani, Kata ya Kipagalo, Mhe. Biteko amewapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji, ambavyo vimepelekea mto Lumakali kuendelea kutiririsha maji ya kutosha.
Katika hatua nyingine Mhe. Doto Biteko amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekusudia kwa dhati kutekeleza mradi huo wa uzalishaji wa umeme, kutokana na ukubwa wake, sambamba na umuhimu wa kuondoa upungufu wa Nishati hiyo hapa nchini ambapo mradi huo wa umeme wa Lumakali utachukua zaidi ya miezi 60 hadi kukamilika kwake utaenda kuongeza megawati zaidi ya 200 katika gridi ya Taifa na kupunguza kabisa shida ya upungufu wa umeme.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka amesema kuwa, serikali inatekeleza miradi mingi ya kimaendeleo kwenye mkoa wa Njombe ikiwemo huo wa umeme, hivyo wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuwasihi wazazi kuwapeleka watoto shule kwakuwa Mhe. Samia amewekeza katika elimu, ambayo ndio Urithi pekee wa Mtoto.
Mara baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Njombe Mhe. Biteko ameendelea na ziara yake Mkoani Iringa na hapo Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Ndugu Deo Sanga alipata nafasi ya kumshukuru Mhe. Biteko kwa kufanya ziara mkoani njombe na akamuahidi kuwa, wao kama chama wanaendelea kusimamia na kuhakikisha ilani ya Chama chama Mapinduzi inaendelea kutekelezwa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.