Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, leo amewatakia heri wanafunzi wote wa Darasa la Nne ambao wanatarajia kuanza mitihani yao siku ya kesho, Oktoba 23, 2024. Katika salamu zake, Mhe. Mtaka amewapongeza wanafunzi hao kwa maandalizi yao na kuwaombea mitihani yenye ufanisi na mafanikio.
Aidha, Mhe. Mtaka pia amewatakia heri wanafunzi wa Kidato cha Pili na Kidato cha Nne, ambao mitihani yao itaanza rasmi mwezi Novemba, 2024. Amewasisitiza wanafunzi hao kutumia muda huu vizuri kwa maandalizi makini ili waweze kufaulu vyema.
Mbali na hayo, Mhe. Mtaka ametoa wito huo kwa wazazi na walezi wote wa mkoa wa Njombe kuwaacha watoto wao wapate utulivu katika kipindi hiki cha maandalizi na mitihani ili wawe na mazingira bora ya kusoma na kufanya mitihani kwa mafanikio.
Mkuu wa Mkoa pia amewapongeza wanafunzi wote kwa kujituma, na kufikisha matarajio yao ya kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atakayepata alama za chini (ziro) katika shule zote za Mkoa wa Njombe.
"Ni matumaini yangu kuwa mtaleta ufaulu mzuri kwenye mitihani yenu na kulifanya taifa letu lijivunie. Tunaamini hakuna ziro kabisa kwenye shule zetu za Njombe," alihitimisha Mhe. Mtaka.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.