Dar es Salaam, Juni 4, 2025 – Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameungana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na waombolezaji wengine katika ibada maalum ya kumuaga marehemu Mzee Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Bikira Maria wa Rozari Takatifu, Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka maeneo mbalimbali nchini waliokwenda kutoa pole kwa familia ya marehemu, akiwemo Mama Mongella pamoja na watoto, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella.
Mhe. Mtaka alitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu na kusisitiza kuwa mchango wa Mzee Mongella katika jamii utaendelea kukumbukwa, hasa kwa kulea kizazi cha viongozi wenye maadili na uzalendo kwa taifa.
Mzee Mongella alifariki dunia Mei 31, 2025 akiwa na umri wa miaka 85, na anatarajiwa kuzikwa jijini Mwanza tarehe 7 Juni 2025.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.