Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana alizindua rasmi mabango yanayotangaza vivutio vya Utalii vilivyopo katika maeneo ya hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Makumbusho ya Taifa.
Mabango hayo yanayohusisha Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Makumbusho ya Taifa - Msitu wa Asili wa Nyumbanitu yamewekwa maeneo ya mzunguko wa barabara kuu mkoani Njombe ili kutoa taarifa za vivutio mbalimbali vya Utalii kwa lengo la kuendeleza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan za kutangaza Utalii hususani mikoa ya Kusini mwa Tanzania.
Leo Septemba 26, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka anapokea viongozi mbalimbali akiwemo Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Mabarozi wa nchi mbalimbali, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Waheshimiwa Madiwani na Wananchi wote wa Mkoa wa Njombe na wa Mikoa yote ya Kusini mwa Tanzania.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.