Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili mkoani Njombe Mei 25, 2024 ambapo hapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka.
Mheshiwa. Biteko anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya kesho Mei 26, 2024 kwenye Uzinduzi wa "Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia" itakayodumu kwa siku kumi Mkoani Njombe kwa lengo la kuwasaidia Wananchi wanaohitaji kupatiwa huduma ya Kisheria.
Mapokezi hayo yameshuhudiwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.