Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, leo 11 Oktoba 11, 2024 amezindua rasmi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, zoezi ambalo linaendelea katika maeneo yote ya mkoa wa Njombe. Uzinduzi huo umefanyika katikaMtaa wa Lunyanywi uliopo Kata ya Mjimwa na kuhudhuriwa na wananchi wa maeneo hayo
Mara baada ya kuandikishwa, Mhe. Mtaka amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuhakikisha wanapata haki yao ya kikatiba ya kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi. Alisema kuwa serikali inaweka mazingira bora na rafiki ili kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura aweze kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi huu muhimu.
"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni nafasi muhimu kwa wananchi kutoa maoni yao kupitia viongozi wanaowachagua. Hii ni sauti ya wananchi katika kuleta maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla. Hivyo, ninawasihi wananchi wote wenye sifa, kuhakikisha wanajiandikisha mapema na kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi," alisema Mhe. Mtaka.
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura linaendelea, na linatarajiwa kufanikisha idadi kubwa ya wananchi wenye sifa kujiandikisha. Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika 27 Novemba 2024
Wajnanchi wa Maeneo hayo waliohudhuria uzinduzi huo wamepongeza juhudi za serikali za kuandaa vizuri mchakato wa uandikishaji na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhakikisha wapiga kura wanafikia vituoni na kujiandikisha kwa wakati.
Mwisho, Mhe. Mtaka alihitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi wote wa Njombe kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo endelevu katika jamii.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.