Katika sherehe iliyofanyika tarehe 12 Desemba, 2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Njombe, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mh. Christopher Ole Sendeka amesema serikali inatambua kuwa lishe ni suala la kimaendeleo hapa nchini na mapambano dhidi ya lishe duni imekuwa ni mojawapo ya maeneo ya kipaumbele katika mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano, 2016/17 hadi 2020/21.
Mchakato wa maandalizi ya mpango mkakati ulishirikisha Halmashauri zote sita na wadau wanaotekeleza shughuli za lishe katika mkoa. Kazi rasmi ya kutayarisha mpango huu ulianza mwezi Oktoba 2018 baada ya kutolewa kwa mpango jumuishi wa taifa wa lishe (National Multisectoral Nutrition Action Plan).
Mkakati umewekwa katika baadhi ya mambo makubwa yafuatayo 1).kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. 2). Kupunguza kiwango cha watoto wanaozaliwa na uzito pungufu 3). Kuongeza kiwango cha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa watoto wenye umri chini ya miezi sita kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo 4). Kuongeza kiwango utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa wanawake wajawazito.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.