Njombe, Julai 28, 2025 — Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amepokea kwa heshima kubwa kitabu cha Malezi ya Watoto kilichoandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili kutoka shule ya sekondari ya Black Rhino Academy International School iliyopo Karatu -Arusha,
Makabidhiano hayo yalifanyika mapema tarehe 23 Julai,2025 ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, ambapo Vivian, alimkabidhi Mhe. Mtaka nakala ya kitabu hicho ambacho kinaelezea namna bora ya kulea watoto katika maadili mema, upendo na nidhamu tangu wakiwa wadogo.
Akizungumza baada ya kupokea kitabu hicho, Mhe. Mtaka alimpongeza Vivian kwa ubunifu na ujasiri aliouonesha, licha ya umri wake mdogo, huku akisema kuwa juhudi zake zinaonyesha kuwa mkoa wa Njombe una hazina ya vipaji vya kipekee vinavyopaswa kutunzwa na kuendelezwa.
“Kitendo hiki si cha kawaida. Ni ishara kuwa vijana wetu wakipewa mazingira mazuri ya kusoma na kuandika wanaweza kufanya mambo makubwa. Vivian ni mfano hai wa kizazi chenye maono,” alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wake, Vivian Frank alisema aliandika kitabu hicho kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa watoto ili kujenga taifa lenye maadili na utu.
Tukio hilo limeibua hamasa kubwa kwa wanafunzi na wadau wa elimu waliopo mkoani Njombe, wakitazama tukio hilo kama chachu ya kuibua vipaji na kukuza utamaduni wa kusoma na kuandika miongoni mwa vijana.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.