Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amefanya mkutano uliotambuliwa kwa kauli mbiu isemayo FUNGA MWAKA BILA KERO katika Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo hapo amesikiliza kero kutoka kwa wananchi wa Makambako na maeneo mengine ya jirani.Akiwa katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi ya Makambako, amewaasa watumishi wa serikali kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea badala yake watambue kuwa wao wanawajibu wa kuwatumikia na kuwahudumia wananchi kwa nafasi zao.
Mhe. Anthony Mtaka amewaeleza wajasiriamali waliokuwa wakichukizwa na baadhi ya watumishi kwenye maeneo hayo kwa kuwazuia kufanya biashara zao sasa wanapaswa kuendelea kufanya biashara zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote na badala yake waruhusiwe kufanya biashara zao masaa 24 na kuzingatia sheria za nchi.
Aidha, katika kuelekea mwaka mpya wa masomo 2024/2025 amewataka wazazi na walezi kuwaandikisha elimu ya awali watoto wote wenye umri unaotakiwa kuanza kusoma na amesisitiza kuwa, kila mtoto aliyepangiwa kuanza kidato cha kwanza ndani ya Mkoa wa Njombe ifikapo Januari 2024 anapaswa kuanza mosomo yake bila kisingizio chochote cha kushindwa kumpeleka mtoto shule.
Sambamba na hayo Mh Mtaka amewahakikishia wananchi kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Daktari Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuendelea kutenga fedha nyingi za maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Makambako hivyo hawana budi kuiunga mkono serikali.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.