Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewataka viongozi wanawake wa Mkoa kuungana Kwa pamoja na kuwa mstari wa mbele kushughulika swala la udumavu Kwa uzito na uharaka kwasababu wananafasi kubwa ya kukutana na wanawake wenzao na kuzungumza nao Kwa ufasaha.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao Cha lishe ambacho kimehusisha viongozi wa Mkoa wa Njombe na Wadau mbalimbali wa maswala ya lishe kutoka mashirika mbalimbali.ambapo amesema kama kutakuwepo na mipango na ufuatiliaji wa mipango hiyo na ushirikiano wa dhati kwa kiwango cha wakazi 800,000 wa Mkoa huu hakiwezi kuwashinda kushughulikia changamoto hiyo.
Huku akiwataka maafisa lishe kuanisha maeneo sahihi yenye udumavu na utapiamlo Kwa kiwango kikubwa ndani ya Mkoa ili kurahisisha mikakati ya kushughulikia ikihusisha viongozi wa dini na kimila
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.