MKUU wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameliomba baraza la mitihani nchini kuwapa mitihani ya kipekee inayoendana na lugha za alama wanafunzi wenye uhitaji maalumu ili kuwaongezea ufaulu.
Ombi hilo limekuja mara baada ya kuibuka hoja ya shule ya sekondari viziwi kushika nafasi ya mwisho mara mbili mfufulizo sababu ikitajwa ni lugha ya kufundishia na lugha ya alama ambayo aina mfanano kama Kiswahili na kingereza,
Akizungumza katika kikao cha tasmini ya elimu mkoa wa Njombe mkuu wa wilaya ya Njombe kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka alisema wanafunzi haowanapata matokeo mabaya kwa sababu kulinga kwa sababu wanashindana na wanafunzi ambao sio wenzao.
‘’Hili ni tatizo haiwezekana watoto wenye mahitaji maalumu kuwapa mitihani sawa na hawa wengine sio sawa..lugha ya kufundishia na lugha ya alama ambayo aina mfanano kama Kiswahili na kingereza’’alisema Ruth.
Mkuu wa wilaya huyo aliongeza kuwa kuna haja ya kuangalia swala hilo upya’’hili linatakiwa kufuatiliwa ili kuwapa wanafunzi hawa nafasi ya kipekee kwa ndio sababu inashusha nafasi ya kimkoa kwa kuwa wanapata ufaulu wa chini mno na wa mwisho kimkoa wamwisho kitaifa na si ajabu wakawa wakwanza kitaifa kwa nafasi yao lakini wanaonekana wa mwisho kitaifa kwa sababu wamechanganywa na wale ambao si washindani wenzao’’alisema Ruth.
Pia mkuu wa wilaya huyo alizungumzia adhabu ya viboko mashuleni kuwa iangaliwe na izingatie sheria na taratibu zilizopo ili isiweze kumuathiri mwanafunzi kwa kumpa kilema cha maisha.
‘’Adhabu ya viboko ni tatizo walimu wanachapa sana..niwaagize maafisa elimu nendeni kwa kustukiza mashuleni walimu wanachapa sana wanafunzi wengine wanawasababishia hadi vilema vya maisha hapana hii aifai’’alisema Ruth.
Hata hivyo afisa elimu mkoa wa Njombe Gifti Kyando alisema katika kikao cha tathimini elimu taifa swala la kulingana kwa mitihani kwa wenye mahitaji maalumu na wanafunzi wa kawaida lilizua mjadalaa katika kikao cha taifa na kwamba serikali imeahidi kulishughulikia na hivyo kuna hatua tayari zinafanyika.
‘’Mh mkuu wa wilaya hiki unachozungumza kuhusu shule za mahitaji maalumu pia kilizua mjadala taifa na serikali imehaidi kulifanyia kazi ili hawa wenye mahitaji maalumu waweze kufanya mitihani yao ambayo itakuwa ya kipekee kulingana na hali zao’’alisema
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.