Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka Leo tarehe 22 Aprili 2024 amekuwa mgeni rasmi katika kikao maalum cha Mafunzo kwa Mawakala wa Mbolea Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania kilichofanyika Mjini Makambako, Kikao hicho kimehudhuriwa na Mawakala kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Morogoro,Ruvuma na Mbeya.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa Mawakala na wauzaji wa Mbolea yameongozwa na Kampuni ya Uzalishaji wa Mbolea ya Minjingu chini na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dokta Mshindo Msolla.
Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na Mawakala hao Amewataka kuacha mara Moja tabia ya uchakachuaji wa mbolea huku akiwataka Mawakala hao kuwa mabalozi wazuri wa kuhakikisha mkulika anapatiwa Mbolea kusudiwa na kwa wakati.
Sambamba hayo amempongeza Bw. Mshindo kwa kuanzisha kiwanda cha mbolea na amemuomba kuendelea na Uzalishaji wa mbolea kwa wingi na kusambaza mbolea hiyo kwa wakulima kwa wakati ili kuondokana na changamoto ya mkulima kucheleweshewa Mbolea.
“Nawapongeza kwa juhudi zenu mnazozifanya kuzalisha mbolea kwa wakulima wetu lakini njooni na mfumo wa kumfikishia Mbolea mkulima kabla ya msimu wa Kilimo kufika hiyo itamuondolea changamoto ya ucheleweshwaji wa Mbolea kwa mkulima” Mhe. Mtaka
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.