• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

Mhe. Mtaka: Njombe Kujikita katika Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na mazao ya Kibiashara.

Posted on: January 11th, 2025

Na. Chrispin Kalinga - Njombe

Njombe, Januari 9, 2025 – Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameendelea na ziara yake ya kikazi akilenga kuimarisha fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu za mazao ya kibiashara. Akiwa katika Kata ya Mtwango, Wilaya ya Njombe, ametembelea shamba la mkulima wa viazi mviringo na kusisitiza umuhimu wa mkoa huo kujikita katika uzalishaji wa mbegu bora za viazi mviringo.

"Tunataka Mkoa wa Njombe uwe mkoa pekee nchini kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zao hili la viazi mviringo, kwa sababu ardhi yetu bado ipo na tena ina rutuba. Hii itatuwezesha kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa ghala la chakula barani Afrika, kama alivyoelekeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan," alisema Mhe. Mtaka.

Rais Samia, katika juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika, alibainisha mikakati mitatu mikuu ya serikali katika sekta ya kilimo: uwekezaji katika miundombinu ya umwagiliaji, kuboresha upatikanaji wa teknolojia na pembejeo za kisasa, na kukuza masoko ya mazao ya kilimo. 

Mhe. Mtaka aliongeza kuwa Njombe inaunga mkono juhudi hizi kwa kuhakikisha inakuwa sehemu ya maghala hayo kwa kuzalisha chakula cha uhakika. Alitoa wito kwa wataalamu wa kilimo mkoani njombe kuja na mbinu mbadala za kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali yanayolimwa Njombe, ili kuongeza uzalishaji na kipato cha wakulima.

"Upatikanaji wa mbegu bora na za uhakika utasaidia kukuza uchumi wa wananchi. Wakulima wengi wa Njombe ni wazalishaji wakubwa wa viazi mviringo, lakini wanajikuta wakipanda mbegu za asili kutokana na uhaba wa mbegu bora. Ni wakati sasa wa kuanzisha mashamba ya kuzalisha mbegu hizi ndani ya mkoa wetu ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya tani 1,000 kwa msimu wa kilimo," alisisitiza Mhe. Mtaka.

Kwa kuzingatia ardhi yenye rutuba na hali ya hewa nzuri, Njombe ina nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali, hivyo kuchangia katika azma ya taifa ya kuwa ghala la chakula barani Afrika

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHE. ANTHONY MTAKA ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MZEE MONGELLA JIJINI DAR ES SALAAM.

    June 04, 2025
  • KATIBU TAWALA NJOMBE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA NANENANE.

    June 04, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE APOKEA MADAKTARI BINGWA 37 KWA AJILI YA HUDUMA ZA AFYA.

    May 26, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI.

    May 23, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.