Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Njombe. Akizungumza Jana Oktoba 06,2024 katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, uliofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mhe. Mtaka alisisitiza umuhimu wa miradi hiyo katika kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.
Katika mkutano huo, Mhe. Mtaka alitumia nafasi hiyo kuwashauri wananchi kuwaheshimu wahudumu wa huduma za afya, akieleza kwamba wao ni watu muhimu katika maisha yetu. "Wahudumu wa afya wanatoa huduma za msingi ambazo ni muhimu kwa ustawi wa jamii zetu," alisema Mhe. Mtaka. Kauli hii inakuja mara baada ya baadhi ya watu kufika kwa muhudumu wa afya kuwajibu vibaya wahudumu hao na kuwarekodi, kisha hutoa taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Mhe. Mtaka alitoa rai kwa wananchi kuwaheshimu wahudumu wa afya kwani ni watu wanaosaidia kuhakikisha tunabaki salama wakati wa mahitaji yetu ya kiafya. "Ni jukumu la kila mmoja kuwapa heshima na ushirikiano wahudumu hao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi," alisisitiza.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.