Kampeni ya Lishe inaendelea ndani ya Mkoa wa Njombe na Mei 02,2024 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka ameendelea na Ziara ya Kukagua utekelezaji wa Afua za Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe ambapo huko ametembelea Mradi wa Shamba Darasa Imara na Ustadi (SADIFU), Mashamba darasa ya Kilimo na biashara (FFBS) pamoja na Bustani zilizoandaliwa katika maeneo ya Shule za msingi kama sehemu ya Wananchi na shule za msingi kujifunza. Pia Mhe Mtaka ametembelea Shule za Msingi ambazo zilifikiwa na Mradi wa SADIFU unaotekelezwa na Shirika la Care international in Tanzania wenye lengo la Uhamasishaji kwa kutoa elimu ya uzingatiaji wa usalama wa chakula na Lishe bora.
Akizungumza mbele ya Wananchi na Wanafunzi katika vijiji vitatu alivyotembelea Mhe. Anthony Mtaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe amewataka wazazi na walezi kuendelea kuzingatia Lishe Bora ili kuondokana na Udumavu kwenye Maeneo yote ya Mkoa wa Njombe.
Kwa Upande Mratibu wa Mradi wa SADIFU kutoka Care international in Tanzania Bi. Liliani Mkusa amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa kutembelea mradi huo huku akiongeza kwa kusema kuwa wao kama Shirika wanaendelea kuboresha mradi waao wanaoutekeleza Mkoani Njombe haswa kuunga Mkono Mikakati ya Kupambana na Udumavu Mkoani Njombe.
Katika Hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitembelea na kukagua mradi unaotekelezwa kwenye Shule ya Msingi Matowo wa Ujenzi wa Madara mawili.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.